Shirikisho la kimataifa la kandanda (FIFA) hatimaye limeondoa marufuku ya shirikisho la soka nchini na kuidhinisha uongozi wa soka kuendelea na shughuli zake. Kenya ilipigwa marufuku mwaka jana baada ya mizozo ya kifedha kati ya wizara ya michezo na uongozi wa soka. Taarifa ya katibu mkuu wa FIFA Fatma Samoura imeelezea kuwa ujumbe wa FIFA utatumwa nchini haraka iwezekanavyo kwa kikao maalum na waziri wa michezo Ababu Namwamba kujadili mustakbali wa soka baada ya amri hiyo ya FIFA.